September 16, 2020


 PATRICK Gakumba, wakala wa mshambuliaji namba moja ndani ya Simba, Meddie Kagere amesema kuwa amepokea ofa nyingi kutoka timu tofauti zikitaka saini ya mchezaji huyo.


Kwa sasa, Kagere amejenga ushkaji mkubwa na benchi kwa msimu wa 2020/21 akiwa hajamaliza dakika 90 ndani ya mechi mbili za ligi ambazo Simba imecheza mpaka sasa.

Mechi hizo ni dhidi ya Ihefu FC ambapo Simba ilishinda mabao 2-1, Kagere alitumia dakika 23 na mchezo wa pili ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Jamhuri, Kagere alitumia dakika 24.

Gakumba amesema:"Kagere bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na utaisha mwakani mwezi wa tano. Mpaka sasa tuna ofa nyingi ambazo zinamtaka mapema ili tusaini mkataba wa awali lakini nawaheshimu Simba na wanakidhi mahitaji yake tulivokubaliana."

Kagere ndani ya misimu miwili akiwa Simba amefunga jumla ya mabao 45. Alifunga mabao 23 msimu wa 2018/19 na alifunga mabao 22 msimu wa 2019/20.

11 COMMENTS:

  1. Mfungaji bora mara 2 mfululizo anawekwa benchi sijawahi ona ndio sasa kwa hii timu yetu yani nasema ubingwa tusahau na huko klabu bingwa raundi ya kwanza tu nje ni upumbavu unafanywa MO atashindwa pesa nyingi anatowa halafu ujinga mtupu

    ReplyDelete
  2. Huyu kocha atatuondolea wachezaji wazuri wengi kwa kuwaweka benchi bilabsababu

    ReplyDelete
  3. kwa msijua na kulaumu kagere alifika mahali mafanikio yakamlevya akawa anajiona yeye ni zaidi ya wenzake hata akiwa kwenye nafac finyu analazimisha kufunga yeye timu inakosa ushindi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Da! nafuu nawewe una jicho kama langu, ilifika mahali wenzake wanaomba mpira analazimisha hata apige na kisigino ilimradi tu

      Delete
    2. Wewe na wenzio wanaokusapoti ni walemavu wa macho na mna akili za kiutopolo tu. Wivu utawaua. Eti kwa wasiojua! �� Mpira unachzwa hadharani kila mtu anaona halafu unataka kumuelekeza nani afikiri kwa matakwa yako? Acha ushamba wewe

      Delete
  4. na hata akikose alikuwa haonyeshi ishara ya kujutia kwa bechi la ufundi na kwa wenza

    ReplyDelete
  5. Halafu ligi ndio kwanza imeanza viherehere vya nini lakini? Mbona tunataka kumwiinglia kocha majukumu yake.Ni mwanzo wa msimu kocha lazima atafute muunganiko unaofaa hasa ukichukulia simba ina wachezaji wengi wenye uwezo hata Charles Ilanfya anaweza kuwa bora kuliko kagere kama atapewa nafasi .Ni kijana ana kasi na anajua kufunga kwanini tusipaze kelele kupewa nafasi hawa vijana. Tanzania hatuna wa michezo tuna watu wenye mihemko.

    ReplyDelete
  6. Haya ndio mambo ya kumwacha Hamisi Tambwe kwa sababu zisizo na msingi ni lini Kagere alijiona anajua zaidi hata kama angekuwa hivyo ni jukumu la kocha kumrekebisha hao mnaowaona wazuri mbona alikuwa anawapita kwa idadi ya magoli

    ReplyDelete
  7. Tusubiri tuone mwisho wa siku mbivu na mbichi openi

    ReplyDelete
  8. Huyu anataka kuipiga simba hela kama anatakiwa na timu zingine ndo uropokeropoke kaa kimya kocha ndo kila kitu

    ReplyDelete
  9. Stephe:; Kocha ndiye mpangaji wateam na ndiye mtaalam, wengine acheni shobo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic