September 5, 2020


 MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri, EFA, Ahmed Shobier amesema kombe la AFCON limepotea katika makao makuu ya Shirikisho hilo.

Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON lilikuwa limehifadhiwa Misri baada ya timu ya Pharaohs kushinda mara tatu mfululizo tangu mwaka 2006 hadi 2010.


Watendaji wa Shirikisho hilo wamedai ya kuwa kombe hilo lilikuwa limehifadhiwa kwa nahodha wa Timu ya Taifa, Ahmed Hassan. Hassan naye amekanusha hilo na kusema alikaa nalo kwa siku moja baada ya kushinda na alikabidhi kombe hilo.


" EFA imeanza kufanya mchakato kwa ajili ya kupata taji lingine na tayari tumeanza kufanya uchunguzi kwa ajili ya kujua lilipo taji la Afcon," amesema Shobier.

 

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic