UONGOZI wa Namungo FC ya Lindi umesema kuwa wapinzani wao Polisi Tanzania ambao mchezo wao wa kwanza walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Azam FC inabidi wawasamehe kwa kuwa wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utanaochezwa Uwanja wa Majaliwa, leo Septemba 14.
Namungo FC inaingia uwanjani ikiwa na rekodi ya kuwa na mfungaji wa kwanza wa bao ndani ya ligi ambaye ni Bigirimana Blaise ambaye aliwatungua Coastal Union wakati wakishinda bao 1-0, Uwanja wa Majaliwa, Septemba 6.
Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema kuwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa leo amesema kuwa hawana namna ya kufanya kwa wapinzani wao wote zaidi ya kusaka pointi tatu.
“Ligi inapoanza huo ni wakati wa kujenga timu, sasa kwa kuwa wapinzani wangu wapo Uwanja wa Majaliwa watatusamehe tu hatuna chaguo zaidi ya kuhitaji pointi tatu muhimu.
“Unapocheza nyumbani ni tofauti kidogo na ukiwa ugenini, tunaanza nyumbani kujenga hali ya kujiamini na tutakapoanza kutoka basi tutakuwa imara zaidi, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti,” amesema Hitimana.
Mchezo wao wa kwanza kwa Namungo kutoka nje ya Lindi itakuwa Septemba 19 ambapo wataibukia Sumbawanga, kumenyana na Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.
0 COMMENTS:
Post a Comment