September 9, 2020


 
UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa kuanza kwa sare ya bila kufungana mbele ya Mtibwa Sugar ni darasa kwao litakalowafanya wayafanyie kazi makosa ambayo wameyaona.

Ruvu Shooting mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 uliochezwa Uwanja wa Gairo, Morogoro ilikamilisha kwa sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90, Septemba 6.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa hawajatishwa na sare hiyo na badala yake wanaendelea kujifunza kwa ajili ya mechi zinazofuata.


"Msimu ndo kwanza unaanza, hakuna tatizo kwetu kuanza kwa sare hilo ni darasa na tunakwenda kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi zetu zijazo.


"Kawaida ushindani ni mkubwa lakini sisi tumeweza kuwa washindani ndio maana tumeweza kupata pointi ugenini haina maana kwamba hatuwezi kushinda hapana mwanzo wa sare kwetu ni darasa.

"Mashabiki wasikate tamaa kwa kuwa ni matokeo ndani ya uwanja, tunaheshimu kila mchezo na kila mchezaji anatambua kwamba lazima atimize majukumu yake ndani ya uwanja na ndio maana hata sasa wapo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu ujao," amesema Masau ambaye pia ni mwalimu. 

Mchezo unaofuata kwa Ruvu Shooting ni dhidi ya Ihefu Uwanja wa Sokoine itakuwa Septemba 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic