September 17, 2020


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amepotezwa mazima na mtangulizi wake wa zamani, Patrick Aussems, ‘Uchebe’ ambaye alimuachia mikoba yake baada ya kupigwa chini msimu wa 2019/20 kwenye mechi mbili za mwanzo ambazo ni sawa na dakika 180.

Sven kwenye mechi zake mbili amevuna pointi nne na kushuhudia timu yake ikifunga mabao matatu huku akipotezwa na rekodi iliyowekwa na Uchebe kwenye mechi mbili ambapo alivuna pointi sita na kushuhudia wachezaji wake wakifunga mabao matano.

Uchebe alifungua pazia la ligi kwa kumenyana na wajeda, JKT Tanzania, Agosti 29 na alishinda kwa mabao 3-1 kisha mchezo wake wa pili ilikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Septemba 13 kwa msimu wa 2019/20 zote zilipigwa ndani ya Uwanja wa Uhuru.

Tayari Simba imecheza mechi mbili kwa msimu mpya wa 2020/21, ilianza kumenyana na Ihefu, Septemba 6 Uwanja wa Sokoine na ilishinda kwa mabao 2-1 na mchezo wa pili ililazimisha sare kwa kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri.

6 COMMENTS:

  1. Uchebe alianzia nyumbani na Sven ameanzia ugenini

    ReplyDelete
  2. Mbona huweki rekodi ya uchebe kombe la FA alilotolewa raundi ya awali mara mbili mfululizo?

    ReplyDelete
  3. Hyu mwandishi anataka kusema Sven hafai hjui mti wenyematunda ndo hupigwa nawe, Sven we kaza buti, Simba mwendo mdundo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anafaa ila angejarbu mifumo tofauti tofauti kulingana na aina ya timu anayochezana na pia ili aweze kuwapa wachezaji wake wote fursa sawa ya kucheza katika kukiimarisha kikosi kizima. Simba inayo mashindano ya CAF akumbuke atahitaji wachezaji karibu wote ili kuendelea na ligi kuu na pia kucheza kimataifa

      Delete
  4. Uchebe kaanzia Nyumbani S Sven away

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic