Na Saleh Ally
KUKOSOLEWA ni sehemu ya maisha ya mwanadamu ambaye anaishi akiwa amezungukwa
na wanadamu ambao kawaida yao ni kuwa na mawazo tofauti. Wanadamu wakati
mwingine wanaweza kukukosoa hata kwa kile wasichokijua kabisa.
Mfano, wewe ni
mtaalamu katika jambo fulani na anayekukosoa hajui lolote lakini ndio mawazo
yake yanamtuma aamini anachofikiri ni kawaida.
Bahati mbaya wako ambao hawajui
lolote na kwa kuwa wana uwezo wa kuzungumza jambo, mfano kupitia mitandao ya
kijamii, badala ya kuingia katika hoja wanaweza kuibuka na matusi, kitu
ambacho hakiendani na hoja za msingi hata kidogo.
Kwa mtu ambaye unabadili
jambo fulani ambalo linahusisha watu, lazima usimame imara na kuendelea
kusonga mbele kwa kuwa unaamini unachokifanya hakiwezi kukamilika ndani ya
siku mbili, tatu au mwaka na unapopitia lazima upite katikati ya lawama,
dhihaka, matusi hadi kufikia unachokihitaji. Wakati unapita huku, kwa woga
huenda kuna wengi wanaweza kukukimbia hata walio karibu yako kwa hofu ya
kuingia katika dhihaka, kejeli na kadhalika na wakawa mbali nawe.
Lakini siku
ukifanikiwa kushinda, siku ya mwisho wataungana nawe na kushangilia pamoja.
Watu wenye kariba ya kiuongozi wananielewa sana kwa mifano hii michache
niliyoitoa na leo ningependa nimguse mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji maarufu
kama Mo Dewji. Huyu ndugu ni shabiki wa Simba bilionea namba moja Afrika kwa
wale vijana kwa mujibu wa takwimu za Forbes.
Amekuwa shabiki wa Simba kwa
miaka mingi, wenye kumbukumbu na mchezo wa soka nchini, wanaweza kuangalia
picha za mwaka 2003 wakati Simba inakwenda kucheza fainali ya Kombe la Caf
baada ya kuitoa Zamalek, wakiivua ubingwa wa Afrika jijini Cairo, wakati huo
ikiwa ndio timu bora Afrika. Mo Dewji alikuwa kati ya Wanasimba walioshiriki
wakiungana na wadau wengine, kiongozi akiwa ni Azim Dewji.
Hii ni kuonyesha
Simba yeye si mgeni, lakini ndoto yake imekwenda mbali hadi aliporejea. Kauli
kadhaa za Dewji ndio zimenifanya kuangalia ndani zaidi, mojawapo ni ile ya
“Siondoki Simba ng’o” akisisitiza kuna watu wanataka kumchanganya ili ajitoe
na kuwafanya wengi wanaomuamini waanze kuumia kutokana na kufeli kwa Simba
lakini ile kauli ya hata watu wa familia yake, wako wanaomshangaa kuona vipi
aendelee na Simba kwa kuwa Simba sasa wala haiingizi faida.
Mo Dewji anaamini
Simba itaanza kuingiza faida baada ya angalau miaka 10 ijayo. Lakini anaona
kuna neema inakuja, ndio maana ameendelea kupambana. Ukiangalia ndani ya
misimu minne, bajeti ya Simba imetoka Sh milioni 560 kwa mwaka hadi takriban
bilioni 7, zaidi ya mara 10.
Kupaa kwa bajeti kunaonyesha kuwa Simba inapiga
hatua kwenda katika ukubwa. Kwa kuwa kila unapolazimika kujitanua kwa bajeti,
maana yake unakua na unalazimika kuwa na mipango thabiti kushikilia ulipo na
uendelee kukua. Kubaki hapo lazima uwe na watu wa uhakika, wafanyabiashara
wanaotambua nini maana ya kusonga mbele, si kazi ndogo, Mo Dewji kajitahidi
sana katika hili. Ubingwa mara tatu: Simba ndio timu mfano na yenye mafanikio
makubwa zaidi katika miaka minne na kumbuka, iko chini ya Mo Dewji.
Mafanikio
haya, lazima uingie ndani na kufanya utafiti, hayawezi kuwa yameshikiliwa na
nguzo za miti mikavu, lazima ni nondo imara kwa maana ya watu wenye maono
jenga na mawazo chanya yenye hesabu sahihi. Mfano: Ukisikia mtu anakuambia
Simba si mfano kwa kila timu ya Tanzania na Afrika Mashariki yote, atakuwa na
roho mbaya au moyo wa kutotaka kujifunza.
Angalia, kila timu leo imelazimika
kuzindua jezi kama Simba, kila timu inatamani au imefanya tamasha linalofanana
na Simba na hata watani wao Yanga ambao ni wakongwe wenzao, wamekopi karibu
kila kitu kilichofanywa na watani wao. Ukiangalia tofauti kati ya Yanga na
Simba katika matamasha yao, utagundua Yanga waliwavalisha wachezaji wao suti.
Zaidi ya hapo unaona mambo yalienda sawa na hili si jambo baya kuigana lakini
vizuri kuongeza ubunifu. Suala la kushindana mashabiki kwa promosheni, Simba
wameanzisha kwa mfumo ambao leo unazivutia klabu nyingi za Tanzania lakini
Afrika Mashariki na hata baadhi ya nchi nyingine za Afrika. Unaona kwa ukanda
wetu kwa sasa, Simba ndio timu inayotajwa sana. Hii ni kutokana na kuwa na
mifumo bora ya uendeshaji inayoifanya kuimarika siku hadi siku.
Kwangu
ukiachana na yale maneno ya Sh bilioni 20 ataweka lini, namchungulia Mo Dewji
upande huu wa pili kwamba, hastahili lawama pekee na badala yake kuna mambo
ambayo amefanya ambayo tunapaswa kuyaona na kuyasema kwa uzuri. Ukichungulia
vizuri, unagundua kuwa kweli kutokana na kuunda mifumo thabiri na watu sahihi
waliojenga timu ya kusaka maendeleo, kuna jambo bora kalijenga ambalo leo
limegeuka kuwa chachu ya mabadiliko na kufanya kuwe na hamu ya maendeleo na
mabadiliko kwa Yanga, Azam FC na kadhalika lakini pia kwa majirani zetu.
Mtu
huyu, hapaswi kupondwa mawe tu. Badala yake, uhuru wa kukosoa tunaweza
kuutumia vizuri kuhoji lakini baada ya kuwa tumepata uhakika wa jambo
tunalohoji kwa kuwa hata kuhoji kunajenga pia lakini kusiwe kule kwa lengo la
ubinafsi. Wakati wa kwenda kwenye mabadiliko ya jambo fulani, makosa hayawezi
kukosekana kwa mwanadamu hata ungekuwa wewe, basi tupongeze na kukosoa ili
tujenge na si kukosoa tu, halafu tukosoe tena, halafu tukosea tena.
MAHASIDI HAWAKOSI SABABU
ReplyDeleteNimekuelewa sana ndugu mwandishi!Ila mpe Salam kigwangala akome kumfuatilia bosi wetu mama mae zake
ReplyDeleteSwadkta Saleh Ally kwa hoja yako ulizotoa na hakika mnyonge mnyongeni na haki yake msisahau kumpatia.
ReplyDeleteKtk biashara kuna mfanyabiashara anayefanya kwa kuzingatia miiko ya biashara kama kuweka mahesabu yake ya mapato na matumizi.Na kuna kwa wale wafanya biashara ambao ni sawa na kenge ktk msafara wa mamba na hawa wanafanya biashara ili mradi aonekane ni mfanyabiashara ambaye hata kumbukumbuku ya mahesabu ya mapato na matumizi haweki ktk vitabu zaidi ya kukuambia biashara asubuhi na mahesabu jioni.Hawana vision ya kupanua biashara zaidi ya matumizi ya kifahari na mwishowe biashara inaanguka kwani hakuwa na misingi imara ya kuzingatia miiko na inabaki kuwa historia kwake kuwa aliwahi kuwa mfanyabiashara tajiri lkn amefilisika.Sababu ya kufilisika hakuwa anafuata miiko ya biashara kama inavyotaka.Kwangu navyoona MO Dewji anataka kwanza kuweka misingi imara na kutufundisha miiko ya biashara ili ataka-poweka huo mzigo wake basi iwe ktk mikono salama.
Lakini wadau wenzangu, mie wakati mwingine napata taabu na kujiuliza huu mzigo wa 20b aliyohaidi MO Dewji hivi inapaswa kuwekwa kwenye bank account ipi? ya Simba Sports Club (wanachama) au Simba Sports Club Company limited ( kampuni)? Kama inapaswa kuwekwa kwenye bnk Acc ya kampuni then itawekwa vipi ikiwa mchakato ( transformation) haujamalizika kama anavyosema mwenye hisa zake 49% ndani ya kampuni.Swali langu la pili ni kwa nini wawakilishi wa upande wa hisa 51% hawatoi mrejesho kinachoendelea/ilipofikia transformation? Na hata wanasheria wa Simba waliohusika na mchakato huu nao mbona hawatupi marejesho na kinachoendelea? Naamini mkiwa na hulka ya kuwahabarisha wanasimba kinachoendelea au mmekwama wapi na sababu zipi basi nafikiri haya mawazo mgando na upotoshaji hatuta-yasikia ambayo ni ya kumkatisha tamaa MO Dewji.
Angalieni nyuma yaliyowafika Yanga wakati wa George Mpondela, Abbas Tarimba, Reginald Mengi na Manji walivyo pigwa vita ya kutaka kufanya mabadiliko ndani ya Yanga ya kuanzisha kampuni na kuishia njiani.Chonde chonde wanasimba kumbukeni Roma haikujengwa siku moja na uvumilivu ni muhimu sana.
Leo CEO wa kwanza wa Simba Magori alitumia muda wa kutosha kupitia kipindi cha sports hq cha redio efm kuelezea kwa ufasaha issue ya billion 20 pamoja na uteuzi wa Barbara ambaye ni CEO wa sasa
DeleteNimekuelewa MO anajua anachokifanya fanya baba tumekupenda wenyew Tim yetu wenyew Unafanya makubwa sana j
ReplyDeletehambay hayakuwepo
Fursa ya kwanza na muhimu kuliko izo 20b.... Mo anataka kuubadilisha mpira kuwa biashara kitu ambacho hakipo Tanzania kwa sasa..... Akifanikiwa ilo tu kwangu nitashukuru.... Maana Timu zingine zitapata darasa na ndipo Mafanikio hayo yatakopokwenda kuwagusa watu wengine wa nje na ndani ya Simba.... Pia kwangu mm 20b sio hoja kihivyoooo.... Hoja tu ni namna gani Simba kama Kampuni itanufaisha wanahisa wake ktk usawa basi.
ReplyDeleteSikilza efm sport hq utapata jibu
DeleteLkn Ingekuwa vizuri pia Kigwa angehoji ni hupi mchango wa wanahisa wenye 51%.... Katika gharama za uendeshaji wa Timu????
ReplyDelete