September 15, 2020

 


KIKOSI cha Yanga, kesho kinatarajiwa kuanza safari kuifuata Kagera Sugar kwa ajili ya kuvaana nao kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

Mchezo huo utakuwa ni wa mzunguko wa tatu ndani ya msimu huu ambao umeanza kwa kasi na kwa raundi ya kwanza pekee yalikusanywa mabao 14.


Yanga inaifuata Kagera Sugar ikiwa imetoka kushinda kwa bao 1-0 mbele ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 13 na bao la ushindi likipachikwa na Lamine Moro dakika ya 86.


Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kikosi kinatarajiwa kuondoka kesho ili kuanza maandalizi kwa ajili ya mchezo huo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba.


Yanga inakutana na Kagera Sugar ambao wametoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina FC Uwanja wa Gwambina na mchezo wa kwanza walipoteza wakiwa nyumbani hapo Kaitaba kwa kunyooshwa bao 1-0 na JKT Tanzania. 

Yanga wao mchezo wao wa kwanza kwa msimu huu walilazimishwa sare wakiwa nyumbani kwa Mkapa kwa kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.

Unatarajiwa kuwa ni mchezo wa kisasi kwa Kagera Sugar ambao mchezo wao wa mwisho msimu uliopita Kaitaba, ilifungwa bao 1-0 na kuyeyusha pointi tatu jumlajumla mbele ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic