September 5, 2020


 UONGOZI  wa Klabu ya Yanga umekanusha vikali taarifa zinazoenea kwamba wameliondoa jina la winga, Benard Morrison kwenye orodha ya wachezaji wao katika usajili uliokamilika hivi karibuni.

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Saimon Patrick amesema timu yao ilipeleka jina la Bernard Morrison kwenye listi ya wachezaji wao wa 2020/21 lakini wameshangaa kuona Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) limeondoa jina hilo na kumuacha kwenye listi ya wachezaji wa Simba.

 

Wakili huyo amesema wao kama Yanga walipeleka jina la Morrison ila wenye mamlaka ambao ni TFF ambao wao wameidhinisha acheze Simba lakini wao wamelipeleka mbele kusaka haki na kesi imeshafika Shirikisho la soka duniani (Fifa) kwa hiyo wana Yanga wasubiri haki yao.

 

Yanga bado ipo kwenye mvutano na mchezaji huyo ambapo kesi ya mkataba wake ilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo TFF na mwisho wa siku Morrison alitangazwa kuwa mshindi.


Ilianza kuskilizwa Agosti 10 mpaka Agosti 12 ambapo ilivuta hisia za mashabiki wengi na wadau wa michezo. Kwa sasa ameshaanza kutumika ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21.


Amecheza mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii, Agosti 30 mbele ya Namungo FC wakati Simba ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku yeye akifunga bao moja na kusababisha penalti iliyofungwa na John Bocco.


Alisaini dili la miaka miwili ndani ya Klabu ya Simba Agosti 8 akitokea Klabu ya Yanga ambayo bado inamtambua kwamba ni mchezaji wao halali.

19 COMMENTS:

  1. Morrison anazichezea akili za viongozi arakavyo. Mnampa kichwa asichostahiki. Mtu katukataa na hatutaki Hana mapenzi na timu na hataki hata kutuona na tayari keshasajiliwa kwengine na kuthibitishwa na FIFA vipi tena tunajitoa thamani kusiko na mfano. Hebu tujaalie tumerejeshewa tunataraji ataipenda timu kwa hiari au kwa nguvu na kulazimishwa kucheza kwa kiwango. Unaweza ukamburura punda mpaka mtoni lakini jee unaweza kumlazimisha kuyanywa maji? Lazima tuwe realidtic haya yakiendelea mwishoni yataweza kuleta athari juu ya timu na naamini kabisa wachezaji tulionao sasa ni bora kuliko huyo Morris anayezichezea akili za waungwana.

    ReplyDelete
  2. Waache tu Yanga wakomae na suala la Morrison kiasi cha kushindwa kufokasi na masuala mengine muhimu. Kama ni kuvurugwa kisaikolojia yanga basi simba wamefanikiwa .kwavuruga yanga KWA Morrison. Simba kuna maangizo kadhaa wapya ila moja ya maangizo bora kabisa simba walioingiza ni Charles Ilanfiya. Kama Ilanfiya atajmtulia na kujiamini kweny nafasi yake ya ushambuliaji basi anaweza kuwa MAGUFULI wa soka ndani ya simba na kuwashangaza wengi kwenye ulimwengu wa soka.

    ReplyDelete
  3. nanukuu maneno ya mh kikwete'"utamaduni wa kuibiana wachezaj simba na yanga upo tangu zamani nanyi yanga mnaweza mkamchukua yoyote toka simba" hapo sis wana yanga tunapoteza muda tu tupambane kwa muda huu kuiweka timu sawa sio kila siku morrison tunakereka

    ReplyDelete
  4. Kama viongozi wa yanga wanampenda sana morisson, wasubiri baada ya miaka miwili wamsaini tena akimaliza mkataba wake simba, vinginevyo kuendelea na suala hili ni ushamba uliopitiliza

    ReplyDelete
  5. Kweli wao hasa walivokusudia na kutokana na hofu waliokuwanazo wakiwa mikono mitupu kwa msimu mitatu ni kuwafanya Simba wapanic, lakini Mnyama Ana akili timamu hayo wanayajuwa na wanawacheka hawababaiki na hila rahisi kama hizo na ubingwa watausikia kwa mashikio to kwasababu ya Niya zao mbaya

    ReplyDelete
  6. Tuwaulize kwanza kama wamemlipia milioni 4 za vibali maana wanalalamika bure

    ReplyDelete
  7. Hapo inaonekana Kuna viongozi wa tff Wana mapenzi timu kubwa na ndio maana Wana maamuzi ya lazima

    ReplyDelete
  8. Yeye au Simba walipe fidia kesi iishe inavyoonesha Yanga hawamhitaji Morrison bali wanamlipa kwa uhuni aliofanya.

    ReplyDelete
  9. We chizi kweli aliyefanya uhuni Morrison au Viongozi wenu wa utopolo nyinyi kama mnajiamini kelele za nini si msubiri maamuzi ya huko mlikoenda sijui CAS ALAFU TUONE mtakavyofungiwa kusajili kwa viongozi kutokujua sheria, Morrison sio chizi kusema hajasaini mkataba na nyinyi

    ReplyDelete
  10. Mlipwe fidia kwa kufoji mkataba na kufutafuta. Kweli Utopolo hamna aibu.

    ReplyDelete
  11. mi nashauri yanga wakiendelea hvi simba wawafungulie mashtaka fifa ya kumgasi mchezaji wao ili iwe fundisho maana Tff wamekubeba kibongo bongo bado unaleta mdomo

    ReplyDelete
  12. Mikia FC mnatoa mapovu na wote mnaongea msichojua....Morisson ana mkataba na YANGA mpaka 2022. Kuwa na mapungufu kwenye mkataba ( as per kamati iliyojipa mamlaka ya kuvunja mkataba wa Morrison na Yanga) hakuufanyi mkataba ule kuwa batili. Tff hii haitoi haki na ngoja tukaitafute mbele

    ReplyDelete
  13. And to add on that....hata kama Morrison hataki kucheza Yanga, twataka utaratibu ufuatwe...

    ReplyDelete
  14. Wengi mnachangia kwa mihemko lakini hamuwazi na kushughulisha akili kidogo tuu.

    ReplyDelete
  15. Wewe unashughulisha ubongo kiutopolo. Uamuzi umeshapitishwa.Hskuna kitakachobadilika.Simba walipita njia hiyo hiyo wakajibiwa na FIFA kwamba hawaingilii maamuzi ya vyama husika. Wakipelekana mchezaji na klabu ndio FIFA hutoa uamuzi. Yanga waliingia choo cha kike kukubali TFF waamue.FIFA hawatabadilisha uamuzi wa TFF.

    ReplyDelete
  16. Ni kweli FIFA haiingilii kabisa maamuzi ya TFF na tulishuhudia hapo nyuma Simba ilipopeleka mashtaka ya kunyimwa points za haki walizonyimwa na baada ya miezi kadha ndio wakajibu kutoyakubali mashtaka ya Simba na kwa upande mwengine tustaajabu kusikia Yanga yatakuwa kujieleza kisa cha kughushi saini ya Morrison ni Kuwa kosa la jinai

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amekudanganya nani kuwa FIFA haiwez kuibgilia maamuzi? Sasa ipo pale kwa ajili ya nn? Kumbe hakuna unachokifaham kwenye soka

      Delete
  17. Hapana alisema FIFA haiwezi kuingilika Bali hayiingili maamuzi ya tff kwasababu ni maamuzi sahihi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic