September 17, 2020

 


KIKOSI cha Yanga leo baada ya kuwasili Bukoba kimefanya mazoezi ya kujiweka sawa ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.


Yanga, Septemba 19 itashuka Uwanja wa Kaitaba kumenyana na Kagera Sugar ambao ni wenyeji kwenye mchezo wao wa tatu ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.


Inakutana na Kagera Sugar ambayo imecheza mechi mbili ikipoteza mchezo mmoja na kulazimisha sare moja pia.


Ilianza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba kisha ikalazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina FC Uwanja wa Gwambina.


Kwa upande wa Yanga yenyewe ilianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons kisha ikashinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City.

    Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic amesema kuwa wachezaji wake wanazidi kuimarika zaidi.


Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo.

5 COMMENTS:

  1. UTO_ Ngja waonje uhondo wa huku mikoani

    ReplyDelete
  2. Msimu uliopita hawakupoteza hata mechi moja huko mikoani. Mechi walizopoteza ni za Dar tu. Ni ngumu sana Yanga kufungwa mikoani.

    ReplyDelete
  3. Mabinngwa wa kihistoria, Daima mbele nyuma mwiko, mikia watateseka sana msimu huu...

    ReplyDelete
  4. Ok lkn hawakufungwa mkoani ikiwemo 2-2 makaburini Bunju Mo Arena

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic