October 18, 2020

 


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa  Arsenal amesema kuwa licha ya  kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana mwamuzi alipaswa aangalie VAR kwa kuwa kulikuwa na dalili ya penalti.


Kipindi cha kwanza mchezaji wa City, Kyle Walker alionekana amepiga shuti karibu na kichwa cha mchezaji wa Arsenal, Gabriel jambo ambalo halikutazamwa kwenye Video maalumu ya kujiridhisha juu ya matukio,(VAR).

Arteta amesema kuwa jambo lile lilipaswa litazamwe kupitia VAR jambo ambalo lilimchanganya kidogo kwa kuwa aliambiwa limetazamwa licha ya kuhoji iliwezekanaje kwa tukio hilo kuchukua muda wa sekunde mbili.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa City Of Manchester, Arsenal ilifanikiwa kupiga jumla ya mashuti matatu yaliyolenga lango huku Manchester City ikipiga jumla ya mashuti matano yaliyolenga lango.


Moja ya shuti ambalo lililenga lango kwa City ni lile lililoleta bao lipigwa na Raheem Sterling dakika ya 23 na kuwafanya Arsenal wayeyushe pointi tatu jumlajumla ugenini.

 

Arteta amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa wachezaji wake kuweza kujilinda baada ya kufungwa bao moja na jitihada zao za kupata pointi ziligonga mwamba hivyo watafanyia kazi makosa yao.





"Ninawapongeza wachezaji wamefanya kazi  kubwa kwa namna ambavyo wamecheza hakuna namna ya kuwalaumu," amesema. 


Arsenal ipo nafasi ya tano baada ya kucheza mechi tano imekusanya pointi 9 na Manchester City ipo nafasi ya 9 ikiwa imecheza mechi nne na pointi zake saba.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic