KLABU ya Mbeya City inayonolewa na Kocha Mkuu, Amri Said imeweka rekodi yake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kucheza mechi sita ambazo ni dakika 540 bila safu yake ya ushambuliaji kufunga bao na safu yake ya ulinzi ikiruhusu kufungwa mabao saba.
Mbeya City ambayo msimu uliopita ilikuwa kwenye hatihati ya kushuka daraja baada ya kubaki ndani ya ligi kwa kushinda mchezo wa playoff kwa kuwa ilimaliza ikiwa nafasi ya 15 na pointi 45 msimu huu kibindoni imejikusanyia pointi mbili pekee.
Pointi hizo Mbeya City ilikusanya kwa kupata sare ya bila kufungana ilikuwa ni mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine na mbele ya Dodoma Jiji kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Ilifungwa mbele ya KMC mabao 4-0 Uwanja wa Uhuru, ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Uhuru,bao 1-0 dhidi ya Azam FC na bao 1-0 dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Sokoine.
Shaha Mjanja, Ofisa Habari wa Mbeya City ameliambia Spoti Xtra kuwa wanajipanga taratibu watarejea kwenye ubora wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment