October 26, 2020

 


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kazi kubwa kwa msimu huu wa 2020/21 ni kuweza kuona inafikia malengo ambayo imejiwekea ikiwa ni kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao wameukosa kwa muda mrefu ama Kombe la Shirikisho.


Azam FC inashika nafasi ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 21 baada ya kushinda mechi saba na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 14 na imefungwa mabao mawili.


Leo Oktoba 26 ina kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri,Morogoro.


Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kazi kubwa ni kufikia malengo ambayo wamejiwekea kwa msimu huu ikiwa ni kupata moja ya taji katika mashindano ambayo watashiriki.


"Msimu uliopita tulianza vizuri ila tukaboronga katikati ilituumiza, kwa sasa tupo vizuri na tunatambua kwamba kuna ushindani mkubwa hilo tunalijua nasi pia tupo kiushindani.


"Ambacho tutakifanya wakati huu ni kuona kwamba moja kati ya malengo yetu ambapo ni kutwaa taji moja kati ya yale mawili makubwa ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara ama Shirikisho kuona kwamba linatimia.


"Mashabiki wazidi kutupa sapoti kwani kila kitu kinawezekana nasi pia tumedhamiria kufanya vizuri kwa msimu huu wa 2020/21." amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic