VINARA wa Ligi Kuu Bara, Klabu ya Azam FC leo Oktoba 26 wamekutana na kisiki cha mpingo baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza ndani ya ligi kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Azam FC ilikuwa imecheza jumla ya mechi saba bila kupoteza na ilifunga mabao 14 huku ikifungwa mabao mawili pekee na kipa wao namba moja David Kissu alikuwa amekusanya jumla ya clean sheet sita kati ya mechi saba.
Leo ameshuhudia nyavu zake zikitikiswa na Jaffary Kibaya dakika ya 62 na kufanya ufalme wake wa clean sheet kuyeyuka huku timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ikiyeyusha pointi tatu kwa mara ya kwanza msimu wa 2020/21.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema :-"Walikuwa wanawaonea wadogo hao Azam FC, leo wamekutana na timu kubwa tukawatuliza."
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:"Haukuwa mchezo wetu tumekwama leo na kupoteza pointi tatu, tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,".
Ndo ligi yenye ushindani unatakiwa iwe hivi.
ReplyDelete