October 18, 2020


BEKI wa Simba, Ibrahim Ame ambaye ni ingizo jipya kwa msimu wa 2020/21 akitokea Klabu ya Coastal Union jana Oktoba 17  ameandika rekodi yake kwa kufunga bao lake la kwanza ndani ya kikosi hicho.


Licha ya kwamba ni beki, kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Mlandege FC ya Zanzibar alipachika bao wakati Simba ikishinda mabao 3-1.


Bao hilo alipachika dakika ya 16 na lilikuwa ni la pili kwa kuwa la kwanza lilifungwa na Chris Mugalu ambaye alipachika mabao mawili kwenye mchezo huo.


Ame alipachika bao hilo kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Luis Miquissone akiwa ndani ya 18.

Bao la kwanza alipachika dakika ya 8 ya mchezo kwa kichwa akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu aliyepiga kona ndefu kwenye mchezo huo na bao la pili ambalo lilikuwa ni la tatu alipachika dakika ya 68 na kuwafanya Simba waondoke uwanjani wakiwa washindi.

Mlandege FC walipata bao dakika ya 71 kupitia kwa nyota wao Yahya Haji aliyemtungua Aishi Manula mazima akiwa nje ya 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic