October 18, 2020


 BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limeipendekeza Tanzania kuandaa michuano ya kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki Mashindano ya Afrika (Afcon) kwa wanawake yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 22 hadi Desemba 6, mwaka huu jijini Dar.

 

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Cacafa, Auka Gecheo, Alhamisi, Oktoba 15 wakati wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya Cecafa kilichofanyika Arusha Jumamosi Oktoba 10 2020, kikao ambacho kiliamua kuendelea na mashindano ya U17 na U20, 2020.

 

Hadi taarifa hiyo inatoka ni mataifa 10, ndiyo ambayo yalithibitisha kushiriki ambayo ni Rwanda, Burundi, Tanzania, Uganda, South Sudan.Mengine ni Sudan, Eritrea, Djibouti, Ethiopia na Kenya.


Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Mirambo amesema: “Ni kweli taarifa hizo zipo na za muda mrefu, awali walitakiwa waandae Sudan lakini mpaka kufikia dakika ya mwisho ikawa imeshindikana, hivyo nafasi hiyo walipewa Tanzania kuandaa mashindano hayo.

 

“Mashindano haya yote ya kufuzu yatashirikisha timu 10 ambazo zitakuwa katika makundi mawili. Baada ya hatua ya makundi, timu mbili za juu zitafuzu kucheza hatua ya nusu fainali," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic