DAVID Kissu Mapingano kipa namba moja wa Azam FC ameweka rekodi ya kuwa kinara wa clean sheet ndani ya Ligi Kuu Bara Bara msimu wa 2020/21.
Azam FC ikiwa imecheza mechi saba amekusanya clean sheet 6 na amefungwa mabao mawili ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Azam Complex wakati Azam ikishinda mabao 4-2.
Jana Oktoba 20, Azam FC ilishinda mchezo wake wa 7 kwa kuifunga mabao 2-0 Ihefu FC na kufikisha jumla ya pointi 21 ikiwa nafasi ya Kwanza Kwenye msimamo.
Kibindoni ina jumla ya pointi 21 na imefunga mabao 14 baada ya kucheza mechi zake 7
Aristica Cioaba, Kocha wa Azam FC amesema kuwa ni furaha kwa timu yake kupata ushindi kwenye mechi zao.
0 COMMENTS:
Post a Comment