MASHINE ya mabao ya Azam FC, Mzimbabwe Prince Dube amefunguka kuwa furaha yake ni kuona timu inashinda kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya ligi.
Nyota huyo amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Azam FC inayofundishwa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba kwa kuwa ni kinara wa kufunga na kutoa pasi za mwisho ndani ya Azam FC.
Pia kiujumla kwenye Ligi Kuu Bara ni kinara wa ufungaji akiwa na mabao sita akifuatiwa na straika wa Simba, Meddie Kagere akiwa na mabao manne.
Dube amesema: “Jukumu letu wote kwa sasa ni kupigana kwa ajili ya timu kuona namna gani itashinda kisha baada ya hapo kila mmoja anafurahi timu inapopata pointi tatu muhimu.
“Kazi yetu ni moja ndani ya uwanja kusaka ushindi bila kujali ni nani atakayefunga ama kutengeneza nafasi ya kufunga ndani ya uwanja, kipaumbele chetu ni ushindi.
"Kwenye mabao ambayo nimefunga mimi wenzangu wananitengenezea nafasi za kufunga ndio maana hata mimi pia ninatengeneza nafasi ili wafunge” amesema Dube.
Azam FC ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi saba na imefunga jumla ya mabao 14.
0 COMMENTS:
Post a Comment