KIUNGO wa timu ya Kaizer Chiefs, Mkenya, Anthony Akumu, ameibuka na
kusema kuwa hana tatizo lolote ikiwa atahitajika katika kikosi cha Yanga kwa
kuwa yeye anachoangalia ni suala la maslahi mazuri kwake.
Akumu ametoa kauli hiyo baada
ya Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya
GSM ambao ni wadhamini wao, Injinia Hersi Said, kuweka picha ya kiungo huyo
katika ukurasa wake wa Instagram kwa lengo la kumtakia kheri ya siku yake ya
kuzaliwa.
Kitendo cha Hersi kuweka picha ya kiungo huyo kwenye akaunti yake ya
Instagram na kumtakia kheri ya kuzaliwa, kimeibua maswali mengi na wadau wengi
wameona kama Yanga wanaelekea kumsajili nyota huyo.
Kiungo huyo alianzia kucheza soka akiwa katika Klabu ya Gor Mahia
kisha akatimkia Al Khartoum ya Sudan kabla ya kujiunga na Zesco United ya
Zambia na mapema mwaka huu akajiunga na Kaizer Chiefs akichukua nafasi ya
aliyekuwa kiungo wa Simba, James Kotei, baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye
timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano mara baada ya picha hiyo katika
ukurasa wa Injinia Hersi, Akumu alisema kuwa kwa upande wake hana shida yoyote
ikitokea atahitajika na Yanga kupitia kiongozi hiyo kwani upande wake hatakuwa
na wasiwasi kwani anajuana naye vizuri.
“Yule ninamfahamu vizuri, sina shida kama atanipa ofa ya kuja Yanga,
kitu kikubwa ni kusikilizana katika suala la maslahi kwa sababu sitaki kubaki
hapa kwa muda mrefu.
“Unajua ligi ya Afrika Kusini ni kubwa lakini hata timu niliyopo pia
ni kubwa lakini haiwezi kuwa sababu ya kushindwa kwenda sehemu nyingine ikiwa
itakuja ofa kubwa kwangu,” alisema Akumu.
Atoke club ya Kaizer chiefs aje yanga? Atakuwa kaona hana future huko.
ReplyDeleteHuo Ni utopolo stone juu ashuke chini, huyo mchezaji atakayefanya hivyo Ni kiazi
ReplyDeleteMbona Luis ametokea huko na sasa anacheza ligi ya ubabaishaji
DeleteLouis katoka timu gani kaja mikia, fraga katoka timu gani kaja mikia. Mikia tunzeni maneno sio kuropoka kama mwarabu wenu wa nguruka
ReplyDeleteImewajaa hofu na kihoro hao, masikio yao kwa wenzao.
DeleteMugalu, Chama walitoka timu zipi hadi kuota mikia?
Okwi alitokaje Esperance de Tunis
Kweli 👆 ww kiazi, utopolo ya mchangani umfananishe na Simba?
ReplyDeleteHamna hela mnafurahisha mitandaoni tu shiboub,kotei,makambo,sure boy wamewashinda kuwasanili mkaishia kuongea tu na bado mnaendekeza siasa za mitandaoni. Kweli ninyi viazi bdo mnamlikia Morrison wekeni bakuli tuwachangie mkanunue hapo wachezaji wawili wanaojua mpira.
ReplyDelete