October 22, 2020


NYOTA wa Simba, Meddie Kagere ametoa kauli ya matumaini kwa kusema yupo kwenye muda wa 'kurikava' majeraha yake ambapo baada ya muda atarejea katika majukumu yake.

 

Kagere ameongeza kwamba kwa kipindi hiki anapumzika kwa ajili ya kujiweka salama baada ya kupata majeraha kwenye mechi iliyopita mbele ya JKT Tanzania.

 

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Simba ilishinda kwa mabao 4-0 huku yeye akitupia mabao mawili.


Straika huyo yupo Dar amekosekana kwenye msafara wa kikosi cha Simba ambacho kipo Sumbawanga na leo Alhamisi kitacheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela.


Nyota huyo mwenye mabao manne amesema kwamba kwa kipindi hiki anaendelea kupata muda wa kupumzika akiuguza majeraha yake ambapo baada ya muda atarudi katika majukumu yake.

 

“Kwa sasa niko kwenye wakati wa kurikava baada ya kuumia, nimepewa siku za kupumzika naamini nitarudi katika mazoezi ya kawaida siku chache baada ya sasa,” alimaliza Kagere.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic