KIKOSI cha Polisi Tanzania kinachonolewa na mzawa, Malale Hamsini leo Oktoba 22 kitashuka Uwanja wa Uhuru saa 10:00 kusaka pointi tatu dhidi ya Yanga.
Malale anakumbukumbu ya kuwaongoza vijana wake kwenye sare ya kufungana na bao 1-1 na Gwambina FC mchezo wake uliopita anakutana na Cedric Kaze raia wa Burundi ambaye leo inakuwa ni mechi yake ya kwanza kukaa kwenye benchi.
Kinara wa utupiaji mabao ndani ya Polisi Tanzania ni Marcel Kaheza akiwa nayo mabao mawili anakutana na Lamine Moro ambaye ni kinara kwa upande wa Yanga akiwa nayo mabao mawili.
Kaheza amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Uwanja wa Uhuru watapambana kupata matokeo chanya.
Lamine Moro amesema kuwa ni mchezo wa kwanza kwa Kaze wanaamini watafanya vizuri wakiwa nyumbani leo.
Kwa msimu wa 2019/20 kwenye pointi sita zilizokuwa zinasakwa kila timu iliambulia pointi mbili.
Mchezo wa kwanza ilikuwa ni 3-3 na ule wa pili ngoma ilisoma 1-1 Uwanja wa Ushirika, Moshi.
0 COMMENTS:
Post a Comment