KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze kibarua chake cha kwanza ndani ya ardhi ya Bongo ni Novemba 22, Uwanja wa Mkapa itakuwa dhidi ya Polisi Tanzania.
Kaze ambaye amesaini dili la miaka miwili Oktoba 16 tayari ameshaanza kukinoa kikosi cha Yanga kwa ajili ya mechi za ligi ambazo zipo mbele yake.
Yanga ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi tano na kujikusanyia pointi 13 inakutana na Polisi Tanzania ambayo ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 10 nayo imecheza mechi tano pia.
Kaze amesema kuwa kwa sasa anahitaji sapoti kutoka kwa mashabiki ili aweze kuwapa kile ambacho wanakihitaji ndani ya uwanja kwa kuwa anaitambua vizuri timu hiyo.
"Nimependa kuja Yanga na ninafurahia kuwa sehemu ya kikosi chenye mashabiki wengi. Ninaona kwamba ili tuweze kufikia mafanikio ni lazima tupeane sapoti katika kazi.
"Mashabiki wanahitaji ushindi hilo ninajua lakini haliwezi kuwa kwa haraka kwa namna ambavyo wanafikira bali ni muhimu kuwa na subira na mambo yatakwenda sawa," amesema.
Novemba 22 tena???
ReplyDelete