October 22, 2020


 TARATIBU siku zinazidi kuyeyuka kuweza kuifikia ile dabi ambayo awali ilipaswa ichezwe Oktoba 18 ila sasa itachezwa Novemba 7.

Kwa sasa ni siku 15 zimebaki kabla ya Yanga na Simba kukutana Uwanja wa Mkapa. Kikubwa kinachotazamwa ni nani ataibuka mshindi.

Hapa mitambo ya kutengeneza mabao ndani ya timu hizo mbili ambayo itakuwa na kazi ya kusaka rekodi mpya namna hii:-

Hawa hapa wa Yanga

Carlos Carinhos

Carlos Carinhos raia wa Angola itakuwa mara yake ya kwanza kucheza dabi.Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 75.

Amehusika kwenye asilimia 40 ya mabao ya Yanga ambayo imefunga mabao saba, amehusika kwenye mabao matatu, akifunga moja na kutoa pasi mbili za mabao ambayo yote yalifungwa na Lamine Moro.

 Ametumia jumla ya dakika 227 ndani ya ligi, dakika 30 mbele ya Mbeya City,35 mbele ya Kagera Sugar 72 mbele ya Mtibwa na dakika 90 Coastal Union.

Deus Kaseke

Mzawa pekee ndani ya Yanga anaingia kwenye orodha ya watengeneza mipango ndani ya timu kwa kuwa alifanya kazi hiyo Uwanja wa Mkapa Oktoba 3, wakati timu yake ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union.

Ametumia dakika 170  ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons dakika 45,Mbeya City 45,Kagera Sugar 35 na dakika 45 dhidi ya Coastal Union.

Tonombe Mukoko

 Mukoko raia wa Congo, alifunga bao la kwanza ndani ya ligi Uwanja wa Kaitaba kwa pasi ya mshikaji wake Tuisila Kisinda wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar. Pasi yake ya alimpa Yacouba Songne wakati Yanga ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkapa.

Amehusika kwenye mabao mawili kati ya 7 ambayo yamefungwa na timu yake kwenye ligi.Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 187.

Mukoko ametumia dakika 375 ndani ya ligi ambapo alitumia 15 mbele ya Tanzania Prisons, dakika 90 mbele ya Mbeya City, dakika 90 mbele ya Kagera Sugar, Mtibwa Sugar 90 na dakika 90 dhidi ya Coastal Union.

                                              

Tuisila Kisinda

Nyota huyu ingizo jipya kutoka AS Vita raia wa Congo ana pasi moja aliyompa mshikaji wake Mukoko kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

Kisinda ametumia dakika 405 ndani ya ligi ikiwa dakika 45 mbele ya Tanzania Prisons, mbele ya Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar dakika zote 90 na Coastal Union alitumia dakika 90.

Ni miongoni mwa wachezaji wenye spidi na uwezo wa kulazimisha mashambulizi ndani ya uwanja itakuwa ni dabi yake ya kwanza.

Katika mabao saba ya Yanga ni mawili yaliyofungwa na Michael Sarpong pamoja na Haruna Niyonzima asisti zake zilikufa baada ya kuguswa na wachezaji wa timu pinzani.

 

Simba hawa hapa

 

Mzamiru Yassin

Kwenye mabao 14 ya Simba amehusika kwenye mabao matatu, amefunga mabao mawili na kutengeneza pasi moja ya bao.Ana wastani wa kuwa na hatari kila baadaya dakika 135.

Alifunga mbele ya Ihefu kwa pasi ya Clatous Chama na kutoa pasi pia kwa John Bocco wakati Simba ikishinda mabao 2-1 na alifunga pia bao moja mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

 Ametumia jumla dakika 406,  dakika 90 dhidi ya Ihefu, dakika 77 dhidi ya Mtibwa Sugar, dakika 90 dhidi ya Biashara United, dakika 90 dhidi ya Gwambina FC na dakika 59 dhidi ya JKT Tanzania.

  

Clatous Chama

Mwamba wa Lusaka amehusika kwenye mabao matano kati ya 14 ndani ya Simba akitumia dakika 433  Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 86.

Ametumia dakika 90 mbele ya Ihefu, alitumia dakika 90 dhidi ya Mtibwa Sugar, alitumia dakika 90 dhidi ya Biashara United, alitumia dakika 86 dhidi ya Gwambina  na kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania alitumia dakika 77.

 

Luis Miquissone

Wanamuita Konde Boy, amehusika kwenye mabao sita kati ya 14 yalifungwa na Simba. Ametengeneza pasi tano na kufunga bao moja mbele ya JKT Tanzania.Ametumia dakika 349.

 

Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 58. Dakika zake alizotumia uwanjani ilikuwa 90 mbele ya  Mtibwa Sugar, dakika 90 dhidi ya Biashara United, dakika 90 dhidi ya Gwambina FC, alitumia dakika 90 na Jdakika 79 dhidi ya JKT Tanzania.

 

Bernard Morrison

Ingizo jipya ndani ya Simba ambaye aliibuka ndani ya mabingwa watetezi akitokea kwa watani zao wa jadi Yanga. Ana pasi moja ya bao alitoa kwa Chris Mugalu wakati Simba ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Mkapa.

Jumla ametumia dakika 194. Dakika zake ni 67 dhidi ya Ihefu, 66 dhidi ya Mtibwa Sugar, 25 dhidi ya Biashara United, 23 dhidi ya Gwambina na 13 dhidi ya JKT Tanzania.

Rarry Bwalya

Kiungo huyu mwenye uwezo mkubwa wa kutumia mguu wa kushoto alitoa pasi moja kwa Meddie Kagere wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Ametumia jumla dakika 247 ilikuwa dakika 90 dhidi ya Biashara United,67 Gwambina FC na 90 dhidi ya JKT Tanzania.

Katika mabao 14 ya Simba ni bao moja la Pascal Wawa lilipatikana kwa mpira wa faulo iliyojaa mazima kambani.Ilikuwa dhidi ya Gwambina FC.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic