October 22, 2020

 


JUA kali lililokuwa likipiga Uwanja wa Uhuru juzi liliwaponza KMC FC, kushindwa kupata ushindi dhidi ya Ruvu Shooting kwa kulazimisha sare ya bao 1-1.

Andrew Vincent, beki wa KMC alifunga bao la kwanza kwenye dakika ya 26 ambapo lilipinduliwa na Shaban Msala wa Ruvu Shooting kwenye dakika ya 56 na kuifanya KMC ifikishe pointi 11 ikiwa katika nafasi ya sita na Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya tisa na pointi tisa.

Ofisa Habari wa KMC FC, Christina Mwagala amesema kuwa changamoto kubwa iliyoikumba KMC kwenye mechi hiyo ni hali ya hewa kutokuwa rafiki kwa vijana wa KMC hadi kuwafanya washindwe kucheza kwa viwango halisi walivyokuwa navyo.

“Hali ya hewa ndiyo iliyoikumba KMC kwenye mchezo dhidi ya Ruvu. Kama unavyofahamu, mechi ilichezwa saa nane, jua la Dar lilikuwa kali mno. Wachezaji walijitahidi kadiri wanavyoweza hadi kufanikisha bao la kwanza, kipindi cha kwanza ila baadaye waliishiwa na nguvu kutokana na hali ya hewa kutokuwa rafiki.

“Hakuna wa kumlaumu kwa kilichotokea. Tumefanya tunavyoweza na tunaahidi kujipanga zaidi kwenye maandalizi ya mechi zijazo ili tuweze kupata ushindi kwenye Ligi Kuu Bara, msimu wa 2020/2021,” alisema Christina.

 

1 COMMENTS:

  1. Mipira ya kibongo ni upuuzi tu, mechi gani inachezwa saa8 mchana! Arafu we mwandishi nae usitudanganye maana kama ni jua lilikuwa haliwaki kwa wachezaji wa KMC tu kwahiyo huo ni ujinga na kukosa la kujibu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic