October 21, 2020


KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji pamoja na mzawa Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi kesho, Oktoba 22 itakosa huduma ya nyota sita wa kikosi cha kwanza.

Simba itamenyana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa kwao ni raundi ya sita baada ya kucheza mechi tano za ligi na Prisons wao watamkosa Salum Kimenya.

Nyota hao ni pamoja na beki Pascal Wawa ambaye yeye yupo zake nchini Ivory Coast na Clatous Chama yupo zake Zambia kwa sasa wote wakifuatilia masuala ya paspoti ili kurejea Bongo kuendelea na majukumu ndani ya timu zao.

 Kiungo Gerson Fraga yeye alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United Uwanja wa Mkapa na beki Ibrahimu Ame hayupo kwenye kikosi kilichopo Rukwa kwa sasa.

Nahodha John Bocco na Meddie Kagere hawa wapo kwenye safu ya ushambuliaji ambapo wanaendelea na programu maalumu zitakazowafanya warejee kwenye ubora wao.

Bocco alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar huku Kagere akipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

Kagere amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri ana aamini kwamba atarejea uwanjani hivi karibuni.

 Kwa upande wa Tanzania Prisons, kiraka Salum Kimenya ana hatihati ya kuukosa mchezo wa kesho kwa kuwa anasumbuliwa na nyama za misuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic