October 21, 2020


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa alitumia miezi sita kuwasoma Simba yenye mastaa kibao ikiwa ni pamoja na Luis Miquissone na Meddie Kagere.

Yanga ina kibarua cha kumenyana na Simba, Novemba 7 Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unasubiriwa na wadau wa mpira ndani na nje ya Bongo.


Kaze amesema kuwa alipokuwa nchini Canada kabla hata ya kusaini Yanga, alipata muda wa zaidi ya miezi sita kuwafuatilia wapinzani wake ambao ni Simba pamoja na timu nyingine ndani ya ligi.

 

“Ukizungumzia ligi ya Tanzania nimeanza kuifuatilia muda mrefu. Miongoni mwa wale ambao nilikuwa ninawafuatilia ni pamoja na Simba, wao najua namna gani wanafanya na mbinu ambazo wanazitumia hivyo sina presha nao pale nitakapokutana nao uwanjani.

 

“Wachezaji wake wengi wapo vizuri hasa ndani ya uwanja na nje ya uwanja pia. Katika hilo, mimi siogopi ndio maana nimekuja kuifundisha Yanga, ninachowaambia mashabiki ni kwamba wasiwe na mashaka katika utendaji wangu,” amesema.


Yanga itawakaribisha Simba ambao ni mabingwa watetezi Novemba 7, Uwanja wa Mkapa mchezo unaoatarajiwa kuchezwa majira ya saa 11:00 jioni.


Msimu uliopita walipokutana uwanjani yalikusanywa jumla ya mabao matano ambapo mchezo wa kwanza, Simba ilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 kisha ule wa pili Yanga ilishinda kwa bao 1-0, zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa.

3 COMMENTS:

  1. Kocha MSENGEE Anapoteza muda kuwaza ujnga

    ReplyDelete
  2. Hawa viazi wanasajili kwaajili ya SIMBA, mwaka watasajili mpaka mashabiki bdo watambwela tu..

    ReplyDelete
  3. akili ni pale unapomtukana kocha bila kosa..
    Akili ni utajir mkubwa kuliko mali, hivi biila hata kufikir unadhan kocha yupo ligi tofauti tena bara jingine aanze kuiwazia simba tena kabla ya hata kusajiliwa na yanga.
    jaman hawa waandishi wanakosa ya kuandika, wanaona bila kuamdika habar za yanga au sba hawauzi magazeti, lkn si kweli kuwa Kaze kasema alikuwa anaiwazia simba.
    kwa hiyo eti tangu mwez March Kaze alikuwa anaifuatilia simba..
    ww mwandishi acha tabia za kike, umbea huo utakuhasi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic