KOCHA Ole Gunnar Solskjaer amekanusha tetesi kuwa staa wake, Paul Pogba yupo njiani kujiunga na Real Madrid, baada ya mchezaji huyo kusema kuwa ana ndoto ya kuichezea timu hiyo.
Pogba ambaye alisajiliwa na Manchester United kwa pauni 89m amekuwa akihusishwa kujiunga na Madrid ambayo inanolewa Mfaransa mwenzake, Zinedine Zidane.
Pamoja na kuwa katika presha kubwa ya timu yake kutocheza vizuri, Solskjaer alipoulizwa juu ya hilo alisema:“Paul ni mchezaji wetu, ataendelea kuwepo hapa kwetu kwa miaka mingine miwili ijayo.
“Tunataka kuona ubora wa Paul, naamini kwa miaka michache ijayo tutashuhudia ubora wake,” amesema Solskjaer na kuongeza:“Tukiwa moja ya klabu kubwa tuna wajibu wa kulinda wachezaji wetu.”
Pogba ametoa kauli hiyo katika mazingira ambayo klabu hiyo haijampa mkataba mpya huku ule wa sasa ukielekea ukingoni na hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika kuhusu mkataba mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment