October 20, 2020


 LEO Oktoba 20 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kutimua vumbi ambapo kutakuwa na timu nane ambazo zitashuka kwenye viwanja vinne tofauti kusaka pointi tatu muhimu.


Mambo yatakuwa namna hii:-Ihefu FC iliyo nafasi ya 17 na pointi zake tatu baada ya kucheza mechi sita itaikaribisha Azam FC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 18 baada ya kucheza mechi sita, Uwanja wa Sokoine.


Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi sita ikiwa na pointi nane itawakaribisha KMC iliyo nafasi ya saba na pointi zake 10 baada ya kucheza mechi sita, Uwanja wa Uhuru.

Mwadui FC iliyo nafasi ya 14 itaikaribisha Mbeya City iliyo nafasi ya 18 ikiwa na pointi mbili baada ya kucheza mechi sita, Uwanja wa Mwadui Complex.

Kagera Sugar iliyo nafasi ya 16 na pointi zake nne baada ya kucheza mechi sita itaikaribisha Dodoma Jiji, iliyo nafsi ya sita na pointi 11 baada ya kucheza mechi sita, Uwanja wa Kaitaba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic