LEO Oktoba 22, Ligi Kuu Bara inaendelea ambapo timu nne zitakuwa kwenye viwanja viwili tofauti kusaka pointi tatu muhimu.
Yanga itakuwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni kumenyana na Polisi Tanzania mchezo wa ligi. Timu ya Polisi Tanzania imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina FC mchezo wao uliopita huku Yanga ikitoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union mchezo wao wa mwisho wa ligi.
Tanzania Prisons itaikaribisha Simba, Uwanja wa Nelson Mandela saa 10:00 jioni, Prisons imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania na Simba mchezo wake wa mwisho ilishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment