October 22, 2020


 LEO, Tanzania Prisons itawakaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni.


Tanzania Prisons wamewaambia Simba kwamba watawafunga leo Uwanja wa Nelson Mandela kwa kuwa wamewafunga mara nyingi.

Rekodi zinaonyesha kwamba mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizi matokeo yao kutotabirika mpaka dakika 90 zitakapokamilika.


Kwa misimu miwili iliyopita wakiwa wamekutana mara nne uwanjani ni bao moja lilipatikana ndani ya dakika 90 huku mechi tatu timu zote zikitoshana nguvu ya bila kufungana.

Matokeo yao ilikuwa namna hii:-2018/19:- Simba 0-0 Tanzania Prisons na mchezo wa pili ikawa Tanzania Prisons 0-1 Simba.

Msimu wa 2019/20 mchezo wa kwanza Simba ilitoshana nguvu ya bila kufungana na Prisons na mchezo wa pili pia matokeo ilikuwa ni Prisons 0-0 Simba.

Salum Kimenya, kiraka wa Tanzania Prisons amesema kuwa wanaamini mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kushinda kwa kuwa wamekuwa wakipata ushindi mara nyingi wanapokutana na Simba.


"Mchezo utakuwa mgumu lakini yule aliyejiaandaa vizuri ndiye atakayeshinda, sisi tumewafunga mara nyingi Simba hivyo hatowahofii tunataka pointi tatu," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Kusema ni rahisi sana ila tunasubiri saa 10 ifike

    ReplyDelete
  2. Huyu ana msongo wa mawazo kipindi kile simba wanamtaka akawa anataka apewe mamilioni yasioendana na kiwango chake sasa jua limekuchwa kiwango kimeisha anabaki kubwabwaja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msongo wa mawazo umehamia kwa mo deuji au mikiani hujui mpira unakariri tu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic