MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru saa 8:00 mchana.
Ruvu Shooting imecheza jumla ya mechi sita na kujikusanyia pointi nane inakutana na KMC ambayo imecheza mechi sita ikiwa nafasi ya saba na pointi 10.
Masau amesema kuwa:"Kikosi kipo imara na tunatambua kwamba mpira wetu sisi ni ule ambao unapendwa na wachezaji wanalijua hilo hasa kwa kutoa burudani ndani ya uwanja.
"Hii ni Barcelona ndogo na inacheza mpira wa pasi ambazo zinaeleweka hivyo mashabiki kwanza wajitokeze kwa wingi uwanjani kuona mpira ule wa pasi unavyochezwa kisha pointi tatu zitakavyopatikana.
"Tunapambana kuona kwamba tunafikia malengo yetu kila kitu kipo sawa hakuna tatizo ambalo lipo ndani ya timu wachezaji wanapenda kuona timu inashinda na ni furaha ya mashabiki wa Ruvu Shooting, hakuna haja ya kuhofia mashabiki wajitokeze," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment