December 18, 2020

 


AZAM FC imekubali sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Desemba 18, Uwanja wa Azam Complex. 

Dany Lyanga alikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 34, bao hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko na kuwafanya vijana wa Charles Mkwasa kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma kwa bao moja.

 Iliwachukua dakika 7 Ruvu kuweka mzani sawa kupitia kwa Emmanuel Martin baada ya kipindi kuanza kwa kufunga bao dakika ya 53 ambalo lilidumu kwa muda wa dakika 7 likapinduliwa na Mudahthiri Yahya dakika ya 60.


Ruvu walitumia dakika 10 kusawazisha bao hilo ambapo dakika ya 70 Fully Zully Maganga aliweka mzani sawa na kufanya ubao usome 2-2.

Ni Idd Seleman kwa Azam FC alionyeshwa kadi ya njano huku wajeda wanne walionyeshwa kadi za njano kutokana na nguvu na spidi ndani ya Uwanja wa Azam Complex.


Hii inakuwa ni sare ya pili mfululizo kwa Azam FC ndani ya Uwanja wa Azam Complex baada ya mchezo wao uliopita kufanya hivyo mbele ya Namungo FC na iligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2.


Langoni alikaa Benedickt Haule na leo langoni amekaa kipa namba mbili, David Kissu na mambo yamekuwa ni 2-2.


Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ibaki nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 16 kibindoni ina pointi 29 huku Ruvu ikiwa nafasi ya nne na pointi 25 nayo pia imecheza michezo 16.

3 COMMENTS:

  1. Jamani Mkwassa anapashwa kupewa hongera nyingi,kocha mzawa anayewasumbua makicha wengi wanaolipwa maoesa kibao,big up mzawa wetu

    ReplyDelete
  2. Makocha wengi wa nje wanavuta mkwanja mrefu pasipo sababu,ifikie sasa tuheshimu vya kwetu

    ReplyDelete
  3. Mkwasa kaenda kuwapa yanga point za bure kabisa. Cha msingi Mkwasa anafanya kazi ya Yanga kuipambania kuchukua ubingwa msimu huu ila letu jucho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic