December 18, 2020



PAUL Scholes na Michael Owen wanaamini kwamba Manchester United wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kuingia ndani ya sita bora kwenye msimamo kwa msimu wa 2020/21.

Ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sheffield United walioupata jana wakiwa ugenini unawafanya wafikishe pointi 23 baada ya kusepa na pointi tatu katika Uwanja wa Bramall Lane. Mabao ya United yalifungwa na Marcus Rashford ambaye alifunga mawili dakika ya 26 na 51 na moja lilifungwa na Anthony Martial dakika ya 23.

Wapinzani wao Sheffield United walipachika mabao yote mawili kupitia kwa nyota wao David Mcgodrick dakika ya 5 na 87. Scholes ambaye ni mchezaji wa zamani wa Manchester United pamoja na Owen wamesema kuwa nafasi ipo wazi kwa timu hiyo kutwaa ubingwa.

Nyota hao wamesema kuwa inawezekana kwa timu hiyo kutwaa ubingwa uliopo mikononi mwa Liverpool ikiwa Kocha Mkuu Ole Gunnar Solskjaer atakuwa na mbinu za kubadili mfumo wa uchezaji kwa timu yake ndani ya uwanja

Scholes  amesema:-"Nadhani ikiwa atabadili mfumo katika uchezeshaji itampa matokeo mazuri hasa ukizingatia ni muda mrefu timu imekuwa ikicheza katika hali ya kawaida tofauti na wakati mwingine. Akitumia mfumo wa 4-2-3-1 unaonekana kufanya kazi kwa timu yake.

"Ni mfumo tu unaonekana kuwa tatizo kwani mpaka sasa bado hajawa na mfumo sahihi na ulio halisi.Umeona namna ambavyo akimtumia Bruno (Fernandes) kuwa namba 10 na kumuweka Martial, Rashford na Mason Greenwood. Inakuwa ni ajabu na inapendeza," .


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic