December 18, 2020

 


BAADA ya ushindi wa mabao 3-2 walioupata Manchester United mbele ya Sheffield United wakiwa ugenini,  Kocha Mkuu Ole Gunner Solskjaer amesema kuwa mabao yote matatu yalikuwa bora na yenye viwango.


David Mcgoldrick wa Sheffield United alianza kupachika bao mapema dakika ya 5 na alipachika bao la pili dakika ya 87 huku yale ya United yakipachikwa na Marcus Rashford aliyefunga mawili dakika ya 26 na 51 na moja lilipachikwa na Anthony Martial dakika ya 33.


Wakiwa ndani ya Uwanja wa Bramall Lane, United ilisepa na pointi tatu na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 23 ikiwa nafasi ya 6 baada ya kucheza mechi 12 huku Sheffield United ikiwa nafasi ya 20 na pointi 1 baada ya kupata sare moja ikiwa imecheza jumla ya mechi 13.


Imeachwa kwa pointi tano na vinara wa Ligi Kuu England ambao ni Mabingwa watetezi Liverpool wakiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 13.


Ole amesema:" Uwezo mkubwa, kila mmoja amepambana na kufanya vizuri, mabao yote ni bora na yenye viwango,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic