LEO Desemba 18, Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Azam Complex.
Ikiwa nafasi ya tatu na pointi 28 inamenyana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya nne na pointi zake ni 24.
Itawakosa nyota watano ambao ni Prince Dube ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Yanga, Uwanja wa Azam Complex, Salim Abubakar,'Sure Boy', aliumia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.
Richard Djod aliumia kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC, Abdalah Sebo aliumia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United na Bryson Raphael aliumia kwenye mchezo dhidi ya Namungo.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wachezaji wawili ambao ni Bryson na Djod wanasubiri ripoti ya kuweza kujua hali zao kama wanaweza kuanza kwenye mchezo wa leo.
Nyota wengine wanaendelea vizuri kwa kuwa wamepata matibabu na wameanza program za kurejea kwenye ubora wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment