KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Desemba 19 kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidiya FC Platinum.
Simba itakuwa na kazi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa nchini Zimbabawe.
Mchezo huo utachezwa Jumatano ya wiki ijayo, Desemba 23 ambapo utakuwa ni wa raundi ya kwanza na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Dar, Januari 6.
Vandenbroeck amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kusaka matokeo chanya kwenye mchezo huo.
Kikosi kilikwea pipa jana Desemba 18 na msafara wa wachezaji 24.
Mwandishi umepatia unahitaji pongezi,
ReplyDeleteImeandikwa Habari fupi imayoeleweka.