January 7, 2021


 LAMINE Moro, beki wa kati wa Klabu ya Yanga ambaye alipigwa chini alipofanya majaribio ndani ya kikosi cha Simba zama za Patrick Aussems kwa anachokifanya kwa sasa ni kama anawaumbua mabosi wa timu hiyo ambao walimkataa.

 

Habari zinaeleza kuwa Aussems ambaye alipewa jukumu la kupitisha jina la beki huyo kitasa raia wa Ghana alilipiga chini jembe hilo kwa kile alichokieleza kuwa uwezo wake ni mdogo.



 

Rekodi za mchezaji mmoja zinaonyesha kuwa Moro ndani ya Ligi Kuu Bara ni kinara wa utupiaji wa mabao kwa mabeki akiwa nayo manne na ana pasi moja ya bao pia ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Cedric Kaze na amempoteza yule wa Simba, Joash Onyango mwenye bao moja.


Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 na kuruhusu mabao 7 ya kufungwa, Moro amecheza mechi 15 na kukosekana kwenye mechi tatu ambapo moja alikosa kwa sababu ya kadi tatu za njano ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania.

 

Mechi 14, ameyeyusha dakika 90 na kumfanya atumie jumla ya dakika 1,260 na moja alitumia dakika 45 nayo kwa sababu aliumia ilikuwa dhidi ya Simba. 


Jumla ametumia dakika 1,305 ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 na timu yake ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kujikusanyia pointi 44 kibindoni.

 

Onyango wa Simba, timu yake ikiwa imeruhusu mabao matano, amecheza jumla ya mechi 14 kati ya 15, ambazo zimechezwa na mabingwa hao watetezi chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.


 Mechi 13, aliyeyuyusha dakika 90 na kufanya atumie jumla ya dakika 1,170 na alitumia dakika 68 kwenye mechi moja hivyo jumla ndani ya Ligi Kuu Bara amecheza mechi 14 na kutumia dakika 1,238.


Timu yake ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza jumla ya mechi 15 ndani ya Ligi Kuu Bara.

4 COMMENTS:

  1. Makanjanja wa Utopolo wanajiliwaza. Platinum ohh Platinum ohh Platinum. Utopolo wanateseka.

    ReplyDelete
  2. Huu ndyo mpira, sio kila mchezaji anafaa kwenye kila timu. Hata angekubaliwa kucheza simba nina uhakika angekuwa hachezi hivi anavyocheza kwa sababu kila timu ina uchezaji wake. Mwangalie Ibrahim Ajib wa Simba na Yanga, Fernando Torres wa Liverpool na Chelsea, Falcao wa Atletico Madrid na Man United nk. Ni wachezaji wachache sana wanawika kila timu wanazokwenda kama Christiano Ronaldo.

    ReplyDelete
  3. Huyo kanjanja hafanyi utafiti kaxi kuropoka tu.Wala sio habari mpya anairudia sana sijui kwa nia gani?
    Kocha wa Simba wakati huo Aussems aliona hafai kwa mfumo wake.
    Move on kanjanja haina umuhimu tena.

    ReplyDelete
  4. Said Maulid SMG alitoka kwao Kigoma kaletwa aje achezee Yanga na alifikia kwa Abeid Mziba. Alipofanya mazoezi kocha Raoul Shungu akamkataa. Kina Mziba wakampeleka Simba kwa kumwomba Rage wakati huo. Akasajiliwa Simba ile fungua dimba msimu huo ikawa Simba na Yanga. Alichofanya Said Maulid Shungu alitamani ardhi ipasuke. Ndipo mwaka uliofuata Said Maulid akarudi Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic