Rais Wa zamani wa Simba, Evans Aveva na msaidizi wake, Geoffrey Nyange Kaburu wamerudishwa gerezani baada ya dhamana waliyokuwa imefunguliwa kwa ajili yao kugonga mwamba.
Jana, Mahakama ya Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam iliwafutia mashitaka ya utakatishaji na kubakiza mengine manane.
Kutokana na kufutiwa mashitaka hayo, dhamana ikawa wazi lakini jana walishindwa kukamilisha masharti, hivyo ilielezwa wangetoka leo.
Hata hivyo, leo Serikali imekata rufaa kupinga wao kufutiwa mashitaka ya utakatishaji hali iliyolazimu hakimu kukubali kusikiliza rufaa hiyo.
Kwa kuwa mahakama imekubali kusikiliza rufaa hiyo Jumatatu, Aveva na Kaburu watalazimika kusubiri hadi hiyo Jumatatu ili kujua majibu ya kusikiliza rufaa hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment