January 12, 2021

 


MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi kwa msimu wa 2020 ni Haruna Niyonzima ambaye ni kiungo mshambuliaji.

Mechi tatu ambazo Yanga imecheza kwenye Kombe la Mapinduzi  imetupia jumla ya mabao mawili kambani na imefungwa bao moja.

Kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri dakika 90 zilikamilikwa kwa ubao kusoma 0-0 Uwanja wa Jamhuri.

Kwenye mchezo dhidi ya Namungo,Yanga ilishinda bao 1-0, mtupiaji alikuwa Zawad Mauya mtengeneza pasi Niyonzima. Kwenye mchezo huu mchezaji bora alichaguliwa kuwa Kibwana Shomari beki wa Yanga. 

 Nusu fainali ya kwanza, dakika 90 zilikamilikwa kwa ubao kusoma Yanga 1-1 Azam FC, mtupiaji kwa Yanga alikuwa Tuisila Kisinda mtengeneza pasi alikuwa ni Niyonzima.Kwenye mchezo huo Noyonzima aliibuka kuwa mchezaji bora.

Yanga ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penalti 5-4 hivyo kesho inakutana na Simba kwenye mchezo wa fainali itakayochezwa Uwanja wa Amaan.

Niyonzima amesema kuwa furaha kubwa ni kuona timu inashinda na kufanya vizuri.

2 COMMENTS:

  1. Kwel ww mwandishi wa habari huna akili kabsa,, unasema mtambo wa mabao yanga n haruna,,wakat Hana hata goli moja! Zaid tu ya pasi mbili,,,,ungejarbu hata kwenda upande wa pil hata Kama sio timu yako,,mechi 3 goli 2 na hakuna mshamvuliaji aliefunga,,wakat Simba mechi 3 goli 7 na yamefungwa na washambuliaji

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hayo ni mawazo yako kwani mantiki yake ni kuhusu kutengeneza nafasi ya magoli na si mfungaji

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic