SELEMAN Matola, Kaimu Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba ambacho leo kitacheza fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Amaan amesema kuwa wachezaji ambao walikosa mechi za awali leo hatawatumia kwenye kikosi cha kwanza.
Mongoni mwa wachezaji ambao walikosa mechi zilizopita ni pamoja na mtambo wao wa mabao, Clatous Chama, raia wa Zambia mwenye pasi nane za mabao ndani ya Ligi Kuu Bara na ametupia mabao sita.
Pia Konde Boy, Luis Miquissone naye hakuwa kwenye kikosi cha Simba kwenye mechi tatu yeye ana pasi saba za mabao na amefunga bao moja kwenye ligi.
Matola amesema:"Fainali itakuwa ngumu kwa kweli hasa ukizingatia kwamba ninakutana na Yanga timu ambayo ni watani wa jadi na inafanya vizuri.
"Hakutakuwa na mpango wa kuwaongeza wale ambao hawakuwa kwenye kikosi mechi zilizopita ikiwa ni pamoja na Chama kwa kuwa haya ni mashindano na yana taratibu zake," .
Et eeh!
ReplyDeleteWaache ufala, Simba na Yanga ni zaidi ya Mashindano.
ReplyDeleteHapo mtu anaenda kuandika record na kumzomea mtani wake. Peleka jeshi lote acheni masihara.
"VIMBURU"Mbona mnaweweseka hivyo!!!
DeleteUTOPOLO hawajui kutofautisha kati ya kuwa serious na kuweweseka
Delete