January 11, 2021


ANAITWA Kelvin Njalubo Moyo ana umri wa miaka 27 raia wa Zimbwabwe amekipiga ndani ya Klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini.


Kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake wa miaka miwili ambao ulitakiwa kumalizika Julai 2021.


Licha ya mchezaji huyo kuwa huru lakini bado amekuwa akiitwa kwenye timu ya Taifa ya Zimbabwe ili aonyeshwe uwezo wake katika kulitumikia taifa.

Mabosi wa Simba wamemuona na kumvuta Bongo ambapo anafanya majaribio ili aweze kupewa dili jipya kabla ya usajili wa dirisha dogo kufungwa Januari 15.


Taarifa kutoka ndani ya benchi la ufundi wa Simba imeweka wazi kuwa bado muda wa kumtazama nyota huo unaendelea hivyo akifikia vigezo wanavyohitaji atapitishwa.

Mtendaji Mkuu wa Simba,(C.E.O) amesema kuwa suala la usajili wa wachezaji wapya limewekwa mikononi mwa benchi la ufundi.

Akiwa ndani ya Klabu ya Chapa United alicheza jumla ya mechi 12 msimu wa 2019 pia ndani ya timu ya Taifa ya Zimbabwe amecheza jumla ya mechi 6 kuanzia msimu wa 2013.

2 COMMENTS:

  1. Waliomwona akicheza huko zenj watupe mrejesho kama atafaa au vipi

    ReplyDelete
  2. Huyu moyo galasa,, hamna kitu kabxa! Viongozi watafute mchezaji mwenye hadhi ya kimataifa. Huyu n wa kawaida sn km kina kihimbwa tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic