IMERIPOTIWA kwamba Manchester United ipo tayari kuingia kwenye vita na Klabu ya Paris Saint-Germain,(PSG) kuwania saini ya kiungo Romain Faivre.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Brest akiwa amecheza mechi 6 na kutupia mabao mawili jambo ambalo limekuwa likiwavutia mabosi wa timu nyingi ikiwa ni pamoja na Manchester United.
Kiungo huyo raia wa Ufarasa msimu uliopita alikuwa anacheza ndani ya Klabu ya Monaco na usajili wake uliwashtua wengi kwa kuwa uligharimu kiasi cha Euro 450,000 kwa ajili ya uhamisho wake.
Kiwango ambacho amekuwa akikionesha ndani ya Brest kimewafanya mabingwa wa Ligue 1, PSG kumtazama kwa ukaribu ili waweze kuwekeza kwake kwa munufaa ya baadaye kwa mujibu wa Le10Sport ambao wameweka wazi kwamba na Manchester United nao wameonyesha nia ya kuwania saini ya nyota huyo.
Ole Gunnar Solskjaer tayari amemjumuisha kiungo huyo kwenye orodha ya wachezaji ambao anawahitaji huku akiingia kwenye vita na Kocha Mkuu wa PSG Mauricio Pochettino ambaye anahitaji pia kufanya kazi na kijana huyo.
Faivre, anatajwa kukubalika kwa kocha huyo wa zamani wa Tottenham ambaye ameanza maisha mapya ndani ya PSG.
0 COMMENTS:
Post a Comment