JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya Klabu ya Simba ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ametaja pale alipo kwa sasa baada ya kuchimbishwa ndani ya kikosi hicho.
Mkude alisimamishwa na Klabu ya Simba, Desemba 28 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu na anatarajiwa kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ili aweze kujibu tuhuma ambazo zinamkabili.
Kwa msimu wa 2020/21, Mkude amecheza jumla ya mechi 10 kati ya 15 ambazo timu yake ilikuwa imecheza jambo linalomaanisha kwamba ni Sven anakubali uwezo wake.
Mkude amesema kuwa yupo ndani ya ardhi ya Dar kwa sasa huku akigoma kuzungumzia sakata lake na Simba.
“Nipo salama kwa sasa ninaendelea vizuri hapa Dar ila kuhusu masuala hayo mengine unayotaka sitazungumza kwa sasa,” amesema Mkude.
Chanzo:Spoti Xtra
Bila simba nani angemjuwa mjinga huyo tena afukuzwe kabisa aende huko kwa hao vyura wenzie
ReplyDeleteEti hiyo nayo mi habari! Duh! Mnateseka sana
ReplyDeleteWakati mwingine kidonda ukikiendekeza huzaa jipu ambalo huleta maumivu makali wakati wa kuliondoa na usipokuwa makini hilo hilo jipu linaweza kusababisha vijipu vidogo vidogo
ReplyDeleteWachezaji wengi vipaji hupotea kwa kukosa nidhamu
ReplyDeleteKweli kbs
DeleteNgoja muharibu mechi na platnum, hamkawii kuja kushutumu uongozi kwa kumuacha mkude. Wekeni akiba ya maneno
ReplyDeleteLeo kila mshabiki wa mikia yupo upande wa uongozi, wskipoteza mechi tu hapo ndio utaona true colors...
ReplyDeleteKwani mkude striker au aseme atalaumiwa akikosekana au anacheza peke yake uwanjani
ReplyDelete