KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametamba kuitumia vizuri michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika nchini Mauritania kuanzia Februari 14 mwaka huu, ili kukaka tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia la vijana.
Julio tayari ameita kikosi
cha wachezaji 40 watakaoingia kambini leo jijini Arusha, ambapo nyota hao
watafanyiwa mchujo mpaka kufikia wachezaji 30 ambao ndiyo watasafiri kwenda
nchini Mauritania kwa ajili ya michuano hiyo.
Akizungumzia mipango yake
kuelekea michuano hiyo, Julio amesema: “Kwanza naweza kusema Watanzania
tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii, lakini tunapaswa pia
kukumbuka kuwa tuna deni kubwa la kuhakikisha tunaisapoti Serikali katika
jitihada zake za kukuza soka hapa nchini.
“Kuhusu mipango yetu kama
benchi la ufundi tuna imani na kikosi ambacho tumekuchagua kwa kuwa nyota wote
waliochaguliwa wana ari ya kupambania utaifa wao na wanajua fika kuwa wakifanya
vizuri ni nafasi kwao kupata timu nje, malengo yetu ni kuihakikisha tunaongoza
kundi letu ili kupata nafasi ya kucheza kombe la dunia,”
0 COMMENTS:
Post a Comment