January 14, 2021

 

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa anaamini uwezo wa mshambuliaji wake, Michael Sarpong ni mkubwa lakini kwa sasa anakwama kufanya vitu vizuri kutokana na kukosa watu sahihi wa kumpa pasi za mwisho.

 

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Sarpong raia wa Ghana, amefunga mabao manne kati ya 29 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayoongoza Ligi ligi baada ya kucheza michezo 18.


Akizungumza na Spoti Xtra,Kaze alisema: “Kwa sasa anapitia kwenye kipindi kigumu kwa kuwa mashabiki wanapenda kumuona akifunga, lakini anashindwa kufunga kwa sababu hapati ile mipira mingi kutoka pembeni jambo ambalo tunalifanyia kazi.

 

“Baada ya muda atakuwa bora na atarejea kwenye ule ubora ambao mimi ninaufahamu kutoka kwake. Wakati unakuja na kila mtu atakubali uwezo wake.“Tatizo hilo nimeanza kulifanyia kazi kwa kutengeneza watu sahihi ambao watakuwa wanampa pasi kutoka pembeni.

13 COMMENTS:

  1. Ipo siku utaondoka nae, endelea kumtetea. Huyo huyo ndie atafanya mazuri yote uliyoyafanya yaonekane si kitu. Ipo siku utaondoka nae.

    ReplyDelete
  2. Kiukweli sarpong anatuangusha sana sina iman kama kiwango chake kitaimarika kwa SASA timu inahitaji performance ya mchezaji so kuvumilia tena

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na maoni ya kocha Kaze,mchezaji anahitaji vitu na mambo mengi hadi kuweza kukaa sawa na kuonesha uwezo wake,tatizo letu wabongo kila mtu ni kocha

    ReplyDelete
  4. Kaze ana maneno mengi Kama zahera. Sarpong anajitutumua tu Ila enzi zake zilishapita. Kama kocha unaona huna viungo sahihi wa kumlisha mbona unaendelea kupendekeza kusajili wafungaji badala ya viungo

    ReplyDelete
  5. Coach yupo sahihi, Ni kweli mchezaji kunakipindi anapitia wakati mgumu, hata Yakouba kama isingekuwa uvimilivu wa Kaze angesha fukuzwa lkn sasaiv anaonyesha uwezo wake, hakuna coach asiependa wachezaji kuperform lkn wakati mwingine kuna mazingira yanapelekea kushindwa kuonesha ubora.
    Hata Makambo mwanzo watu walimdharau lkn akawa tishio

    ReplyDelete
  6. Hakuna kocha anaeponda wachezaji wake Ila Kaze anajua kuwa Sarpong hamna kitu. Ligi imefika mzunguko wa pili bado mnasema avumiliwe

    ReplyDelete
  7. Watu wanao sema Sarpong avumiliwe aendelee kubakia wengi ni mashabiki wa simba na wanajua Sarpong ni mzigo hana manufaa yoyote kama mshambuliaji na kama mnamtaka basi simba wamchukue hata bure maana atawasaidia sana klabu bingwa. Tujiulize kwanini Rayon Sports walimvunjia mkataba? na sababu zilizotolewa kuwa ni utovu wa nidhamu ni za kweli? kama alikuwa mfungaji mzuri Rayon si wangemvumilia? na kwanini baada ya kuachwa Rayon alikuwa huru bila timu yoyote? APR hawakumuona wamsajili. Mashabiki uchwara mashabiki maandazi mkiambiwa ukweli mnasema eti " Kanjanja" Makanjanja ni nyie msie kubaliana na hali halisi. Sarpong amechangia kushusha kiwango cha Waziri Junior, leo Waziri atatolewa kwa mkopo kwenda Coastal Union na kule mpaka msimu unaisha atakuwa na goli zisizo pungua 10 na huyo Sarpong mnaetetea aendelee kuwepo Yanga mtashuhudia atakuwa na goli ngapi, kwa utabiri wangu hatazidi goli 6 mpaka ligi inaisha. Huu ni mzigo Yanga fanyeni maamuzi au na nyie " mmelogwa kama Sarpong? ". Alimtukana rais wa Rayon fc na watu wakamwendea kwa wataalam kama Morrison anavyocheza mpira akiwa benchi. This is African Magic.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona alivyokuja mlimpokea kama mfalme, au hayo yote mmeyajua leo

      Delete
    2. Hahahaa eti African magic. kumbe ndo kazi yenu kuroga wachezaji, hovyo kabisa. Mngeroga mchukue club bingwa aftica

      Delete
    3. Bro Leo hazard hafungi kule Madrid je ni mzigo naeye??wewe ndio hujui mpira unakurupuka tu nikumbushe CHIRWA huyu alicheza mechi 13 bila kufunga watu wakamuita mzigo baadae alikuja kuzoea mazingira akawa Bora hata wale waliomkejeli mwanzo wakataka KUMSAJILI na Leo bado yupo mwalimu anajua tatizo la timu ndio maana amesema ivo pia huyo wazuri sijui unamsifia kwa lipi waziri alikua Azam wakamtema kaenda mbao kapata bahati Leo Yuko yanga anapewa nafasi haonyeshi leo mirji ambae hakua anapewa nafasi kawa mfungaji Bora waziri anaruka ruka bado unamjadili??tuwe fare tuheshimu taaluma za watu

      Delete
  8. Kama mnatunza kumbukumbu vizur, Kaze kabla hajawasili yanga alisema ameifuatilia timu na amegundua tatizo ni viungo. Muda wote huo mpaka leo amependekeza kiungo gani asajiliwe

    ReplyDelete
  9. Sarpong ni tatizo kaze kama kumbadilisha inawezekana fanya hivyo kabla mambo

    hayajawa mabaya zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic