IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wapo kwenye kukamilisha dili la usajili wa mshambuliaji mmoja raia wa Congo Ferebory Dore, anayetajwa kama pacha wa Said Ntibanzokiza ‘Saido’, baada ya wadhamini wa Yanga, kampuni ya GSM, kukamilisha dili la usajili wake.
Straika huyo wa zamani wa timu ya Angers ya Ufaransa, sasa Yanga wamesema kuwa atatua Visiwani Zanzibar kwa ndege ya moja kwa moja.
Yanga tayari ilishawasilisha jina la Dore kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Hersi Said, tayari ameshafanikisha kuliteka soko la Dore na kukamilisha dili hilo.
Mbali na Dore hivi karibuni pia Eng Hersi alikaririwa akisema yupo pia kwenye mazungumzo na nyota wao wa zamani Heritier Makambo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 26, ambaye Agosti 10, mwaka jana alijiunga rasmi na Klabu ya Horoya AC ya Guinea, katika mkataba unaotarajiwa kufikia ukingoni mnamo Jun 30 mwakani.
Pamoja na mkataba huo kutarajwa kufikia kikomo mwakani, bado thamani yake kwa sasa inatajwa kufikia Milioni 319 ambapo amefanikiwa kucheza mechi za kimataifa 13, huku akifunga mabao matatu na kusaidia kufunga bao moja ndani ya dakika 718.
Pia imeelezwa kuwa kwa sasa mabosi hao wa Yanga wanaoambania suala la vibali kwa ajili ya wachezaji hao.
"Kuna surprise kubwa inakuja Zanzibar, siku hizi chache ambapo timu itakuwa kwenye michuano ya Mapinduzi Cup, kikubwa nikuombe ueendelee tu kuwa mtulivu, kwani tunahitaji kuleta straika mapema iwezekanavyo ili aweze kujumuika na kikosi na mara baada ya Mapinduzi tu awe amezoea tayari kwa kutoa msaada wake kwenye ligi.
“Dhamira msimu huu ni kutwaa kombe, hivyo matumaini yetu makubwa ni kuhakikisha tunaona siku za hivi karibuni tunamtambulisha straika atakayeweza kutusaidia katika suala la upachikaji wa mabao,” kilisema chanzo chetu.
Kuhusu usajili wa Yanga, Injinia Hersi amesema:"Kila kitu kipo sawa na kuna mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa ambaye atatambulishwa hivi karibuni,".
Nyie hamuwachi maporojo yenu ya kila siku mitambo mipya mitambo mipya huku mapya hatuyaoni tunayaona mapya ya Mikia lakini wao kimyakimya bila ya makeleke yasiyokwisha bila ya mapya isipokuwa sare zisizokwisha
ReplyDeleteSawa boss wa gsm
ReplyDelete