UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na Simba kumewaumiza kwa kuwa haikuwa malengo yao kwa msimu wa 2020.
Mtibwa Sugar ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila, msimu wa 2019 ilitwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.
Kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ambaye anashughulikia vibali kabla ya kuanza kukaa kwenye benchi rasmi ambapo kwenye mechi za Kombe la Mapinduzi, Vincent Barnaba alikuwa akisimamia mechi hizo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wameumizwa na matokeo waliyopata ila hawana chaguo la kufanya.
"Kikosi kilikuwa imara na tulikuwa tunahitaji kutwaa ubingwa kwa mara nyingine kwa kuwa tumepoteza hatuna chaguo tutapambana kwa ajili ya wakati mwingine.
"Matokeo hayakuwa mazuri kwetu na kwa sasa tumerejea Morogoro na kuvunja kambi ikiwa ni kwa ajili ya kuwapa mapumziko wachezaji wetu.
"Tutarudi kambini mapema kuanza kujiweka sawa kwa ajili ya ngwe ya pili ya Ligi Kuu Bara ambayo tunaamini kwamba itakuwa na ushindani mkubwa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment