January 13, 2021



KUELEKEA mchezo mkali wa fainali ya kombe la Mapinduzi utakaopigwa leo kwenye dimba la Amani visiwani Unguja na kuzikutanisha Simba na Yanga, Yanga wamemuongeza mshambuliaji Saido Ntibazonkiza kikosini.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Simba na Yanga kukutana msimu huu ambapo kumbukumbu ya mwisho kwao ni sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Novemba 7, mwaka jana.  

Simba imeingia kwenye fainali hiyo baada ya kuwaondosha Namungo kwa kuwachapa mabao 2-1 katika hatua ya nusu fainali huku Yanga wao wakiiondosha Azam kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 5-4 katika hatua hiyo.

Kuelekea mchezo huo kuna uwezekano mkubwa wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ kuivaa Simba, hii ni baada ya taarifa za daktari kuthibitisha kuwa amepona majeraha yaliyomfanya akose michezo ya awali.

Akizungumza kuhusu hali ya nyota huyo Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema: “Kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba, hatuna majeruhi yoyote zaidi ya Yacouba Sogne ambaye aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Azam, lakini anaendelea vizuri na tuna matarajio makubwa atakuwa sehemu ya mchezo lakini tunasubiri ruhusa ya Daktari.

“Kuhusu, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ yeye hakucheza michezo iliyopita kutokana na kuwa na majeraha lakini kwa sasa yupo vizuri na kama kocha ataona inafaa anaweza kumtumia,"



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic