January 3, 2021


NYOTA wa Klabu ya Yanga, Wazir Junior yupo kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kutokana na kukosa nafasi kikosi cha kwanza.

Junior ambaye ni ingizo jipya aliibuka huko akitokea Klabu ya Mbao FC ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka msimu wa 2019/20.


Timu mbili zinatajwa kupeleka barua kumpata nyota huyo kwa mkopo ili kupata huduma yake ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 yenye ushindani mkubwa.


Ihefu FC inayonolewa na Zuber Katwila inaelezwa kuwa iliwahi mapema kupeleka barua ya kumuomba nyota huyo kwa mkopo ila mpaka sasa mabosi wa Yanga wamewachunia.

Pia timu nyingine ambayo inahitaji huduma ya nyota huyo ni Coastal Union ya Juma Mgunda ambayo nayo pia inatajwa kupeleka barua ya kuhitaji saini yake.

Ndani ya Yanga inayoongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18, Wazir amecheza mechi mbili.

Pia kwenye mabao 29 ametupia bao moja ilikuwa dhidi ya KMC wakati timu hiyo ikishinda mabao 2-1, Uwanja wa CCM Kirumba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic