January 6, 2021

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Januari 6 kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Simba imepata matokeo hayo ikiwa nyumbani na kufanikiwa kupindua meza kibabe baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kufungwa bao 1-0.

Bao la kwanza, Uwanja wa Mkapa lilifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 39 kwa mkwaju wa penalti baada ya Shomari Kapombe kuchezewa faulo ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti. 

Licha ya wachezaji wa FC Platinum kuonekana wakilalamika mwamuzi aliamuru ipigwe penalti na bao la pili lilifungwa na Shomari Kapombe dakika ya 62.

Bao la tatu ilikuwa ni John Bocco dk 90+1 na msumari wa nne ni Clatous Chama kwa penalti dakika ya 90+5 na kuifanya Simba itinge hatua ya makundi.

Wakiwa ugenini walifungwa na Perfect Chikwende ambaye leo aliwekwa kwenye uangalizi wa Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ambao walikuwa wakibadilisha kuweka ulinzi ndani ya Simba.

Sera ya WIDA,(War In Dar) imekubali baada ya Simba kupndua meza kwa kuwa FC Platinum ya Norman Mapeza ilipania kumaliza mchezo huu Uwanja wa Mkapa ila mambo yalikuwa magumu kwao.


Kazi ya kwanza imekamilika sasa ni kazi kwenye hatua ya makundi ambayo ina ushindani mkubwa kutoka timu kubwa ambazo zimewekeza mkwanja mrefu.

9 COMMENTS:

  1. Kilichonifurahisha ni kuwa safari hii timu ya kigeni haikupata sapoti kama ilivozoeleka na huu ni mwanzo mpya na tuendelee kushirikiana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Weee...ngoja simbaipangw3 na AS Vita, utawaona haooo

      Delete
    2. Walikuwepo wachache tena wakiwa wametinga jezi za Utopolo

      Delete
  2. Mungu ibariki nchi uetu Tanzania, Mungu ibariki Simba

    ReplyDelete
  3. Tanzania ina bahati moja pekee kwenye mashindano ya CAF ndio nchi pekee katika wakati huu wa CORONA inaruhusiwa kuingiza mashabiki uwanjani ....hii inafanya inakuwa kwenye faida kwenye mashindano....nadhani nchi nyingine watapeleka malalamiko kwani wanakuwa kwenye unfair advantage...wachezaji wa timu pinzani wanapopimwa na kukutwa na CORONA hawachezi sasa nasubiri kuona hii faida itaendelea kwenye hatua za makundi ama CAF watarekebisha kanuni zao wakati huu wa CORONA....ili kutoa "usawa" katika mashindano kwa nchi ambazo zimeathirika na CORONA????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo sio issue, hata Ulaya Kuna viwanja mashabiki wanaingia na hii ni kutokana na rate ya maambukizi kuwa chini. Kwa hiyo hiyo sio issue na tufurahie matokeo yetu mazuri!

      Delete
  4. Al Lec Utopolo utakuuwa.Simba alishinda Nigeria kulikuwa na watazamaji?
    Nani alikuwa na advantage?Roho inakuuma. Focus kwenye timu yako wscha sweeping reasons zisizo na kichwa wala miguu.

    ReplyDelete
  5. Wachezaji wanapimwa hata Ulaya. Ulitaka ifanyike nini?Wacha husda na ujinga wa kiutopolo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic