January 6, 2021

 




MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman leo Januari 6 amepokea zawadi ya jezi ya Yanga baada ya kufanya ziara Ofisi za Ikulu ya Zanzibar.

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela,alibeba jukumu la kutoa zawadi hiyo baada ya msafara wa Yanga kutembelea Ofisi ya Ikulu ya Vuga,mjini Unguja.


Msafara wa Yanga ulikuwa pamoja na wachezaji na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye anakinoa kikosi hicho kinachoongoza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa sasa kikosi kipo Zanzibar baada ya kuweka kambi huko kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mchezo wa kwanza ilicheza jana na kikosi cha Jamhuri na Yanga ilitoshana nguvu ya bila kufungana ndani ya dakika 90.

3 COMMENTS:

  1. Ila mwakalebela nae apunguze tumbo, ndio maana kuna wakati anakuwa kama anakosa mantiki

    ReplyDelete
  2. Hawa kandambili kazi yao kugawa jezi kwa wapemba hao mambingwa wanawakilisha nchi wengine walikuwa uwanjani wanawashangilia zimbabwe akili nywele niamini sasa wawasindikize airport kesho

    ReplyDelete
  3. Yanga Ndiyo timu ya Wananchi, ikulu Ni nyumbani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic